Timu ya Millwall ikiwa na wachezaji
kumi imefanikiwa kupata ushindi wa dakika za mwisho dhidi ya mabingwa
watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza Leicester City na kutinga hatua ya
robo fainali ya kombe la FA.
Timu hiyo ya ligi ya daraja la
kwanza ilishuhudia beki wao Jake Cooper akitolewa nje katika dakika
ya 52 ya mchezo kwa kucheza rafu na kupata kadi mbili za njano.
Hata hivyo Shaun Cummings, alifunga
goli pekee katika mchezo huo baada ya kuinasa pasi ya Lee Gregory na
kuwapita mabeki wa Leicester kisha kuachia shuti la chini lililompita
Ron-Robert Zieler.
Shaun Cummings akiangalia mpira alioupiga ukimpita kipa na kujaa wavuni
Mchezaji wa Leicester City Bartosz Kapustka akijaribu kufunga kwa tiki taka
Wakati huo huo timu ya Huddersfield
imelazimisha sare tasa dhidi ya Manchester City katika mchezo
mwingine wa kombe la FA uliopigwa katika dimba la John Smith, matokeo
ambayo yanaufanya mchezo huo kurudiwa ili kupata mshindi.
Kipa Claudio Bravo, aliyeanza katika
kikosi hicho aliokoa michomo mara mbili kutoka kwa washambuliaji
Rajiv van La Parra na mpira wa adhabu uliopigwa na Jack Payne, huku
goli la Philip Billing likikataliwa kwa kuotea.
Kocha Pep Guardiola akimtolea hasira zake mchezaji Fabien Delph
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni