Real Madrid imeendelea kuwa kileleni
mwa Ligi Kuu ya Hispania La Liga, mbele ya Barcelona, baada ya kupata
ushindi dhidi Osasuna katika mchezo ulioshuhudia tukio baya la kuumia
mchezaji Tano Bonnin.
Mchezaji huyo beki wa timu hiyo
iliyomkiani mwa La Liga alivunjika mguu, wakati akikabiliana na
mchezaji Isco wa Real Madrid, katika kipindi cha kwanza cha mchezo
huo.
Cristiano Ronaldo alikuwa wa kwanza
kutumbukiza mpira uliompita kipa, Salvatore Sirigu na kuwafanya
wageni Real Madrid waongoze kabla ya Sergio Leon kusawazisha goli.
Isco aliuwahi mpira uliokuwa
ukizagaa langoni mwa Osasuna na kufunga goli la pili la Real Madrid,
na kisha baadaye Lucas Vazquez akafunga goli la tatu katika dakika za
mwisho na kufanya matokeo kuwa 3-1.
Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kufunga goli la kwanza la Real Madrid
Kiungo Mhispania Isco akifunga goli kwa utulivu baada ya kuunasa mpira uliokuwa ukizagaa langoni mwa Osasuna
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni