Sadio Mane ameibeba Liverpool na
kuitoa katika kufanya vibaya hivi karibuni baada ya kufunga mara
mbili ndani ya muda wa dakika mbili katika kipindi cha kwanza na
kuizamisha Tottenham Hotspur kwa magoli 2-0.
Mshambuliaji huyo raia wa Senegal
aliifanya timu ya Liverpool kuongoza alipokimbia na kuiwahi krosi ya
Georginio Wijnaldum na kupachika goli wavuni katika dakika ya 16 ya
mchezo huo.
Mane akaongeza goli la pili sekunde
138 tu baadaye kwa kujipinda na kuachia shuti la karibu kufuatia
mpira uliokuwa ukizagaa katika goli la Tottenham, baada ya kipa Hugo
Lloris kuzuia michomo ya Adam Lallana na Roberto Firmino.
Mshambuliaji Sadio Mane aliyechini akifunga goli la kwanza la Liverpool
Sadio Mane akijipinda kufunga goli la pili la Liverpool katika mchezo huo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni