Rais wa Marekani Donald Trump na
mgeni wake Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe wameelekea Mar-a-Lago kwa
ajili ya kucheza gofu na kufanya mikutano yao.
Rais Trump ameungana na mkewe
Melania Trump, ambaye alikuwa amevalia koti na blauzi nyeusi, suruari nyeupe
na mawani ya jua wakati akipanda ndege ya Air Force One.
Binti wa Trump, Ivanka na mumewe
Jared Kushner nayo walikwea kwenye ndege ya Air Force One katika
safari hiyo.
Kutoka kushoto Melania Trump, rais Trump, Waziri Mkuu wa Japan Abe na mkewe wakipunga mkono kuaga kuelekea Mar-a-Lago
Rais Trump, mkewe Melania na mgeni wake Shinzo Abe na mkewe wakiwasili Mar-a-Lago
Rais Donald Trump na mgeni wake Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe wakipata mlo wa mchana katika Ikulu ya Marekani
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni