Watu wapatao 17 wamekufa katika
tukio la kukanyagana kwenye uwanja wa mpira kaskazini mwa Angola
katika mji Uige.
Mamia wameripotiwa kujeruhiwa wakati
mashabiki wa soka walipovamia geti baada ya kuzuia kuingia ndani ya
uwanja, kutokana na uwanja kujaa.
Baadhi ya mashabiki walioanguka
walikandamizwa chini na kufa kwa kukosa hewa katika tukio hilo
lililotokea jana.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni