Rais Donald Trump anapanga kutoa
agizo lake jipya la kuwapiga marufuku raia wa baadhi ya mataifa
kuingia Marekani, baada ya jaribio lake la awali kuzuiliwa na
mahakama.
Bw. Trump amewaambia waandishi wa
habari akiwa kwenye ndege ya rais Air Force One, kwamba agizo hilo
jipya atalitoa mapema jumatatu ama jumanne.
Uamuzi huo wa Trump umekuja baada ya
mahakama ya rufaa ya San Francisco kukazia uamuzi wa mahakama ya
chini kuzuia agizo lake.
Agizo la rais Trump lililenga kupiga
marufuku kuingia Marekani raia wa mataifa saba ya Kiislam.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni