Watu waliojitolea nchini New Zealand
wamefanikiwa kuwarejesha kwenye kina kirefu nyangumi 100 kati ya 400
waliojikuta wakikwama kwenye kina kifupi cha maji.
Wengi wa nyangumi hao walikufa
katika kisiwa cha kusini, baada ya kukaa muda mrefu nje ya maji,
lakini kwa nyangumi walionusuriwa sasa wanaogelea baada ya kuokolewa.
Mamia ya wakazi wa kisiwa hicho
walifanikiwa kuokoa maisha ya nyangumi hao 100, kwa kuwasukuma hadi
kwenye kina kirefu cha maji.
Watu wakishirikiana kumsukuma nyangumi kuelekea kwenye maji ya kina kirefu
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni