Wakala wa Wayne Rooney, Paul
Stretford, yupo nchini China kuona kama anaweza kufanya makubaliano
ya mshambuliaji huyo kuhamia Ligi Kuu ya China.
Hakuna uhakika wa kufanikisha mpango
huo, huku ikionekana kwamba mpango huo hauwezi kufanikishwa kabla ya
kufungwa kwa dirisha la uhamisho Februari 28.
Hata hivyo kutokana na ukweli kuwa
Stretford amesafiri kwenda China, inaashiria wazi kuwa kocha wa
Manchester United, Jose Mourinho atamruhusu Rooney, 31, kuondoka.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni