Zoezi la upimaji wa Afya Bure kwa wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani linalofanyika kuanzia jana, linaendelea katika viwanja vya Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba Ilemela.
Mchungaji wa kanisa hilo, Dkt. Daniel Moses Kulola amebainisha kwamba jana zaidi ya wananchi 150 walijitokeza kupima afya zao ambapo zaidi ya 70 walihudumiwa na kurejea nyumba.
Alisema zoezi hilo limejikita kwenye uchunguzi wa afya ya uzazi, kisukari, presha pamoja na uzito likiongozwa na wataalamu wa afya kutoka Canada wanaosaidizana na wataalamu wazawa. #BMGHabari
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni