Timu ya Arsenal imejikuta ikipata
pigo katika matumaini yake ya kuwani ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza
baada ya kupata kipigo cha kushtukiza cha magoli 2-1 kutoka kwa
Watford, ikiwa ni ushindio wao wa kwanza dhidi ya Arsenal tangu mwaka
1988.
Beki wa zamani wa Tottenham Younes
Kaboul alifunga goli la kwanza la Watford katika dakika 10 tu ya
mchezo huo kwa shuti ambalo mpira wake ulimgonga Aaron Ramsey na
kutinga wavuni.
Baada ya kupita dakika mbili na
sekunde 57 wageni Watford waliongeza goli la pili lililotumbukizwa na
Troy Deeney akiunganisha mpira wa Etienne Capoue. Arsenal walipata
goli pekee lililofungwa na Alex Iwobi.
Younes
Kaboul akishangilia kwa kunyanyua mikono juu baada ya kufunga goli la kwanza
Mchezaji Troy Deeney akifunga goli la pili la Watford
Alex Iwobi akifunga goli pekee la Arsenal katika mchezo huo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni