Mama mtu mzima aliyejifungua mtoto
akiwa na umri wa miaka 72, amekiri kuwa hali yake ya kiafya imekuwa
sio nzuri tangu ajifungue mtoto huyo.
Mama huyo Daljinder Kaur, 73, aishie
Amritsar, huko Punjab, kaskazini mwa India, alijifungua mtoto wake wa
kwanza Aprili 19, mwaka jana, lakini tangia hapo amekuwa na shinikizo
la damu na viungo vyake kudhoofika.
Mtoto wake huyo wa kiume Armaan kwa
sasa ameanza kutambaa, licha ya mama yake huyo kikongwe kuacha
kumnyonyesha baada ya miezi mitatu.
Mume wa kikongwe aliyejifungua mtoto akiwa amembeba mtoto wao
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni