Arsenal waliobakia kumi wametolewa
katika Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 kwa mara ya saba mfululizo
baada ya kufungwa kwa ujumla wa magoli 10-2 na Bayern Munich katika
michezo yote miwili.
Katika mchezo wa jana Arsenal ambayo
mchezo wa awali ilifungwa magoli 5-1 nchini Ujerumani, ilipata goli
la kwanza kupitia kwa Theo Walcott katika dakika ya 20, kabla ya
Bayern kupatiwa penati iliyosababishwa na Laurent Koscielny.
Robert Lewandowski aliitupia penati
hiyo wavuni na kusawazisha goli, kisha Arjen Robben akafunga goli la
pili, Douglas Costa akafunga goli la tatu na kisha baadaye Arturo
Vidal akafunga la nne katika dakika ya 80 na kuongeza la tano dakika
ya 85.
Theo Walcott alikuwa wa kwanza kufunga goli katika mchezo huo
Robert Lewandowski akisawazisha goli kwa mkwaju wa penati
Laurent Koscielny akipewa kadi nyekundu na kutolewa nje
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni