Real Madrid imetokea kufungwa goli
moja nyuma dhidi ya Napoli katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya
Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora na kutinga robo fainali kwa kuibuka
na ushindi wa magoli 3-1.
Napoli iliyotawala sehemu ya nusu ya
kwanza ya mchezo huo ilipata goli la kuongoza katika dakika ya 24
wakati Dries Mertens alipoifungia Napoli goli la kwanza baada ya beki
ya Real kupoteana.
Hata hivyo Kapteni Sergio Ramos
alisawazisha goli hilo na kisha kusababisha lingine la kujifunga la
Mertens na kisha baadaye Alvaro Morata alifunga kwa kufuata shuti la
Cristiano Ronaldo na kukamilisha ushindi.
Dries Mertens akishangilia baada ya kufunga goli
Kapteni wa Real Madrid Sergio Ramos akiupiga kichwa mpira uliosawazisha goli
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni