.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 3 Machi 2017

ATLETICO MADRID YASEMA TORRES ANAENDELEA VIZURI BAADA YA KUANGUKA VIBAYA UWANJANI

Atletico Madrid imesema mshambuliaji wake Fernando Torres anaendelea vizuri baada ya kugonga kichwa chini baada ya kuanguka katika mchezo ulioisha kwa sare ya 1-1 na Deportivo.

Mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool na Chelsea ambaye bado yupo hospitali alianguka vibaya baada ya kugongana hewani jana usiku na Alex Bergantinos katika dakika ya 85.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania, 32, atafanyiwa vipimo zaidi hii leo, licha ya Atletico kusema vipimo vya scan havijaonyesha kuumia vibaya.
                            Fernando Torres akiwa amelala chini baada ya kuangukia kichwa
Wachezaji wa Atletico Madrid wakimsaidia Torres kwa kuuvuta ulimi wake asiumeze

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni