Mahakama Kuu nchini Zimbabwe imepiga
marufuku kitendo cha kuwapiga watoto mashuleni na hata majumbani
nchini humo.
Uamuzi huo wa Mahakama umetolewa
kufuatia mzazi mmoja kulalamika mtoto wake darasa la kwanza mwenye
miaka 6 kupata michubuko baada ya kuchapwa na mwalimu.
Mzazi Linah Pfungwa amesema mtoto
wake wa kike alipigwa na mwalimu kwa kusahau kitabu chake kusainiwa
na mzazi kuthibitisha amefanya kazi aliyopatiwa kuifanya nyumbani.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni