Barcelona imeweka historia katika
Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuwa timu ya kwanza kubadili matokeo ya
kufungwa magoli 4-0 katika mchezo wa kwanza na kuibuka na ushindi wa
magoli 6-1 katika mchezo wa marudiano.
Timu hiyo ya Hispania ilikuwa na
matokeo ya jumla ya kufungwa magoli 5-3 katika dakika ya 88 ya
mchezo, lakini ikageuza matokeo kwa kufanikiwa kufunga magoli matatu
katika dakika saba za mwisho wa mchezo huo uliopigwa Nou Camp.
Goli la Neymar la shuti la mpira wa
adhabu na la penati lililofuatiwa na goli la Sergi Roberto katika
dakika ya 95 yalitosha kuipatia ushindi usiotabirika Barcelona na
kusonga mbele katika michuono hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Barcelona ilikuwa ikiongoza kwa
magoli mawili kwa bila kupitia mpira wa kichwa wa Luis Suarez na
Layvin Kurzawa kujifunga la pili na kisha baadaye Lionel Messi
aliongeza la tayu kabla ya Edinson Cavani kuchomoa goli moja.
Mpira wa kichwa uliopigwa na Luis Suarez ukijaa wavuni na kuandika goli la kwanza
Neymar na Luis Suarez wakiondoka golini na mpira baada ya kufunga goli
Mshambuliaji Edinson Cavani akifunga goli pekee la PSG katika mchezo huo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni