Pierre-Emerick Aubameyang amefunga
magoli matatu wakati Borussia Dortmund ikiichakaza Benfica kwa
magoli 4-0 na kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Wenyeji wa Borussia Dortmund
walikuwa nyuma kwa goli 1-0 waliofungwa katika mchezo wa awali,
walisawazisha matokeo kupitia kwa Aubameyang katika dakika ya nne kwa
kichwa.
Dortmund waliongeza la pili kupitia
kwa Christian Pulisic, kisha baadaye Aubameyang aliyekosa penati
mchezo wa kwanza akaongeza la tatu na kufunga la nne dakika ya 85.
Pierre-Emerick Aubameyang akifunga goli la kwanza kwa mpira wa kichwa
Pierre-Emerick Aubameyang akiendeleza mvua yake ya magoli hapo jana
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni