.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 9 Machi 2017

WANAWAKE KUTOKA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA WASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Wanawake wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) wakiungana na mamia ya wanawake wengine duniani, kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani, iliyofanyika kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.
Siku ya Wanawake Duniani iliadhimishwa jana kwenye viwanja vya Mwem be Yanga Jijini Dar es Salaam, ambapo wanawake kutoka Ofisi za serikali na binafsi waliungana na wenzao kusherehekea siku hiyo muhimu. Pichani ni wanawake kutoka Idara mbalimbali za Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) wakifurahia siku hiyo.

Wanawake kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wakiserebuka kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam, wakiifurahia siku ya Wanawake Duniani iliyoadhimishwa jana, ambapo mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.
Wanawake wakiwa kwenye furaha wakiadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, iliyoadhimishwa jana katika viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam, ikiwa na kauli mbiu ya Tanzania ya Viwanda; Wanawake ni Msingi wa Mabadiliko ya Kiuchumi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni