Watu 13 wamekufa na wengine watatu
wamejeruhiwa baada ya basi la kanisa lililokuwa limewabeba watumishi
waandamizi wa kanisa kutoka mkutano wa kujitathimini kugongana gari
aina ya pick-up nchini Marekani.
Ajali hiyo imetokea jana majira ya
saa 12:30 nje kidogo ya Garner State Park, maili 75 magharibi mwa San
Antonio, Texas.
Mamlaka za Texas bado hazijaeleza
kama wote waliokufa walikuwa kwenye basi hilo la kanisa ama kwenye
gari la pick-up.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni