Cristiano Ronaldo amefunga magoli
mawili katika dakika za mwisho wakati Real Madrid ikitokea nyuma kwa
magoli 3-1 na kutoka sare katika mchezo ambao Gareth Bale alitolewa
nje dhidi ya Las Palmas katika dimba la Bernabeu.
Isco aliipatia Real Madrid goli la
kuongoza katika dakika ya nane, kala ya Tana kusawasisha kwa shuti
kali.
Mshambuliaji wa Wales gareth Bale
alionyeshwa kadi nyekundu katika kipindi cha pili kwa kumsukuma
Jonathan Viera ambaye allifunga kwa mkwaju wa penati baada ya Sergio
Ramos kuushika mpira.
Kevin-Prince Boateng aliifunga Real
Madrid goli la tatu kabla ya Ronaldo kufunga goli kwa mpira wa penati
na kisha baadaye akafunga kwa kichwa na kupelekea kugawana pointi na
Las Palmas.
Mchezaji raia wa Wales Gareth Bale akionyeshwa kadi nyekundu
Cristiano Ronaldo akifunga kwa kichwa goli na kufanya matokeo kuwa magoli 3-3



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni