Timu ya Manchester City imetinga
robo fainali ya kombe la FA baada ya kupambana kutoka nyuma baada ya
kufungwa goli moja na Huddersfield na kuibuka na ushindi wa magoli
5-1.
Katika mchezo huo wa marudio baada
ya kutoka sare tasa, Leroy Sane na Pablo Zabaleta walibadili matokeo
kwa kufunga magoli na kisha Sergio Aguero kuongeza la tatu kwa mkwaju
wa penati.
Aguero tena akatumbukiza golini
krosi ya Raheem Sterling na kuandika goli la nne na kisha baadaye
Kelechi Iheanacho akafunga la tano katika dakika ya mwisho za mchezo
huo.
Mchezaji Leroy Sane akifunga goli la kwanza na Manchester City
Kelechi Iheanacho akifunga goli la tano katika dakika ya mwisho ya mchezo



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni