Timu ya Barcelona imeichakaza
Sporting Gijon kwa magoli 6-1 katika mchezo wa Ligi ya Kuu ya
Hispania ya La Liga na kukwea pointi moja nyuma ya vinara wa ligi
hiyo timu ya Real Madrid.
Katika mchezo huyo wa jana ambapo
kocha wao Luis Enrique alitangaza kuachana na timu hiyo katika msimu
wa joto, Lionel Messi alifunga goli la kwanza kwa kichwa na Juan
Rodriguez ajakijifunga.
Carlos Castro alifunga goli na
kufanya matokeo kuwa magoli 2-1, lakini Luis Suarez na Paco Alcacer
wakaongeza magoli mengine kabla ya Neymar naye kufunga kwa mkwaju wa
adhabu na Ivan Rakitic kukamilisha karamu.
Lionel Messi akiupiga kwa kichwa mpira uliozaa goli la kwanza
Luis Suarez akiwa amewapiga chenga mabeki hadi kipa na kufunga goli



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni