.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 25 Machi 2017

ITALIA YASHINDA LICHA YA VURUGU ZA MASHABIKI WA ALBANIA

Ushindi wa Italia wa magoli 2-0 dhidi ya Albania ulisubiri kwa dakika nane baada ya mashabiki wa Albainia kurusha fashifashi na mabomu ya moshi katika dimba.

Katika mchezo huo kipa wa Italia, Gianluigi Buffon alicheza mchezo wake wa 1,000, huku wakipata goli la kuongoza kupitia kwa mkwaju wa penati ya Daniele de Rossi.

Urushaji wa fashifashi ulifanyika kwanza wakati De Rossi akipiga penati, lakini ilikuwa katika kipindi cha pili ambapo wachezaji walilazimika kutoka uwanja katika mchezo huo wa kuwania kufuzu kombe la dunia.
               Daniele de Rossi akimpoteza mahesabu kipa wa Albania na kufunga goli
           Immobile akiangalia mpira aliopiga ukijaa wavuni na kuandika goli la pili 
Mashabiki wa Albania wakiwa wamewasha fashifashi na kurusha mabomu ya moshi uwanjani
Kipa wa Italia Gianluigi Buffon akinyanyua mikono juu kuwashukuru mashabiki kwa kutimiza mchezo wake wa 1,000

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni