Manchester United imetoa sare
ugenini na FC Rostov katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Uropa hatua
ya 16 uliochezwa nchini Urusi.
Katika mchezo huo United walipata
goli muhimu kupitia kwa Henrikh Mkhitaryan aliyefunga kwa shuti la
karibu kufuatia kazi nzuri ya Zlatan Ibrahimovic.
Ibrahimovic aliachia shuti
lililogonga mwamba katika kipindi cha pili kabla ya Aleksandr
Bukharov kunasa pande la Timofei Kalachev na kusawazisha goli.
Henrikh Mkhitaryan akifunga goli na kuifanya Manchester United kuongoza
Aleksandr
Bukharov akisawazisha goli na kufanya matokeo kuwa 1-1
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni