Mashabiki wapatao 200 wa timu ya
Arsenal wameandamana na mabango jana usiku katika uwanja wa Emirates
kushinikiza kocha wao Arsene Wenger ajiuzulu.
Wanachama hao wa Arsenal wanataka
uongozi wa klabu hiyo kutomuongezea kocha Wenger mkataba mpya huku
wakisema anaiuwa klabu hiyo.
Usiku wa jana ulijidhihirisha kuwa
ni janga kwa Arsenal na kwa kocha Wenger baada ya kufungwa magoli 5-1
na timu ya Bayern Munich.
Mashabiki wa Arsenal wakiandamana na bango lililoandikwa "Kila hadithi nzuri inamwisho wake" ikiwa ni ujumbe kwa kocha Wenger
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni