.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 8 Machi 2017

WANANCHI WASHANGAA MABOMBA KUTOA MAJI YA PINKI CANADA

Mamlaka ya mji wa Alberta nchini Canada imewaomba radhi wananchi baada ya maji ya bomba yaliyowekwa dawa kubadilika na kuwa na rangi ya pinki.

Wakazi wa eneo la Onoway katika mji wa Alberta, waliwasilisha malalamiko yao kwa mamlaka ya mji buo baada ya mabomba yao kuanza kutoa maji yenye rangi ya pinki siku ya jumatatu.

Meya wa Albert, Dale Krasnow, ameutoa hofu umma na kusema maji hayo hayana madhari kwani hali hiyo ilitokana na kemikali ya kutibu maji ya Potassium permanganate.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni