Rais Donald Trump amempigia simu
rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ikiwa ni simu yake ya nne kupiga kwa
kiongozi wa taifa la Afrika tangu aingie madarakani.
Katika maongezi yao yaliyofanyika
jana mchana, viongozi hao wameahidi kuimarisha ushirikiano baina ya
mataifa hayo mawili.
Simu ya kwanza ya Trump kwa kiongozi
wa Afrika ilikuwa ni baina yake na rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari
ambapo walizungumzia masuala ya tatizo la ugaidi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni