Mechi ya kimataifa baina ya Ivory
Coast na Senegali imeisha kabla ya muda kutokana na kitendo cha
mashabiki kuvamia uwanja.
Refa wa mchezo huo alilazimika
kumaliza mpira katika dakika ya 88 kutokana na hali kuwa mbaya
kutokana na mashabiki.
Katika mchezo huo mshambuliaji wa
Liverpool Sadio Mane alifunga goli kwa mkwaju wa penati, hata hivyo
Cyriac Gohi Bi alisawazisha dakika mbili baadaye.
Shabiki aliyevamia uwanja akiwa amemrukia Lamine Gassama
Shabiki aliyekuwa bila shati akikimbizwa na walinzi baada ya kuvamia uwanjani
Walinzi wakimdhibiti shabiki aliyekuwa amevamia uwanjani




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni