Mtoto wa marehemu Etienne
Tshisekedi, kiongozi wa upinzani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,
amechaguliwa kutwaa wadhifa wa baba yake.
Felix Tshisekedi, 53, sasa ataongoza
mazungumzo muhimu ya muungano wa upinzani ya mustakabali wa kuondoka
madarakani rais Joseph Kabila.
Chini ya makubaliano yaliyofikiwa
mwaka jana, uchaguzi mpya utafanyika mwishoni mwa mwaka 2017, na rais
Kabila hatogombea uongozi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni