Kozi hiyo iliyoendeshwa na Wilfred
Kidao - Mkufunzi anayetambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu
Afrika (CAF), itafungwa saa 5.00 asubuhi kwenye Viwanja vya Michezo
vya Bandari, vilivyoko Tandika jijini Dar es Salaam.
Mbali ya Kidao, wakufunzi wengine
walikuwa ni Manyika Peter aliyefundisha programu au mtaala kwa
makocha wa makipa; Dk. Nassoro Ally Matunzya aliyewanoa makocha hao
kuhusu tiba za wanamichezo/wanasoka na Mkufunzi wa muda mrefu wa
soka, Hemed Mteza.
Wanafunzi wa kozi hiyo wanaotarajiwa
kuhitimu kesho Jumatatu ni pamoja Doris Malyaga ambaye ni Mwanamke
pekee kati ya wanafunzi 27 walisoma kozi hiyo kwa kipindi cha siku 14
cha mwanzo wa mwaka. Doris ni mwanahabari za michezo aliyehudhuria
kozi hiyo. Anaandikia gazeti la MwanaSPOTI linalotolewa na Kampuni ya
Magazeti ya Mwananchi (MCL).
Wengine ni nyota wa zamani wa timu
ya mpira wa miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ waliopata kuchezea
klabu kongwe na kubwa nchini. Wanafunzi hao ni Boniface Pawasa, Fred
Mbuna, Innocent Haule, Herry Morris, Ivo Mapunda, Nizar Khalfan na
Mussa Hassan Mgosi.
Wengine ni Omar Kapilima, Amosi
Mgisa, Uhuru Mwambungu, Yussuf Macho, George Minja, Haruna Adolf,
Selemani Omari, Ally Ruvu, Masoud Selemani, Haji Mustapha, Mhasham
Khatib, Issa Ndunje, Salum Kapilima, Said Salum, Julio Elieza, Hassan
Mwakami, Rajab Mponda, Ally Mbonde na Evod Mchemba.
..…………………………………………………………………………........................
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA
MIGUU TANZANIA (TFF)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni