Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini
amemfukuza kazi waziri wake wa Fedha, Bw. Pravin Gordhan baada ya
siku kadhaa za uvumi wa kuchukua uamuzi huo ulioathiri soko na fedha
ya nchi hiyo.
Nafasi ya Bw. Gordhan itachukuliwa
na Malusi Gigaba imesema taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Rais Zuma
jana.
Mapema wiki hii rais Zuma alimuagiza
waziri Gordhan kurudi nchini na kutohudhuria tukio lililokuwa
lifanyike Uingereza.
Katika mabadiliko hayo Sfiso
Buthelezi atakuwa Naibu Waziri wa Fedha akichukua nafasi ya Mcebisi
Jonas.
Kumekuwapo na shinikizo la kumtaka rais Zuma ajiuzulu


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni