Timu ya Wanawake ya Manchester City,
imekuwa timu ya kwanza ya Uingereza kutinga nusu fainali Ligi ya
Mabingwa Ulaya tangu mwaka 2014 baada ya kuifunga Fortuna Hjorring.
Mabingwa hao wa Supa Ligi,
waliwafunga goli 1-0, timu hiyo ya Denmark katika mchezo wao wa
kwanza na kuongeza ushindi wao kwa kufunga tena kwa goli la Lucy
Bronze.
Caroline Rask alipoteza nafasi nzuri
ya kufunga huku Mchezaji Bora wa Mwaka Duniani Carli Lloyd akipiga
shuti lake nje.
Mpira wa kichwa uliopigwa na Lucy
Bronze ukimshinda kipa na kujaa wavuni


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni