Rubani wa ndege ya shirika la ndege
la American Airlines amefariki dunia wakati ndege aliyokuwa
akiiongoza ikitokea Dalllas kwenda Albuquerque, New Mexico.
Ndege hiyo aina ya Boeing 737-800
ilikuwa katika umbali wa maili mbili kabla ya kutua pale rubani
alipowasiliana na uwanja wa ndege kuomba msaada wa dharura wa
matibabu.
Ndege hiyo ilitua salama, wakati
abiria wakikaribia geti la uwanja walipishana na madaktari waliokuwa
wakikimbilia kwenye ndege kutoa msaada.
Shirika la ndege la American
Airlines limethibitisha kutokea kwa kifo cha rubani wake huyo
aliyetambulika kwa jina la William "Mike" Grubbs.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni