Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akiongea na wamiliki wa
vyombo vya Habari (hawapo katika picha) wakati wa mkutano wa Wadau
Tuzungumze kuhusu namna vyombo vya habari vinavyoshiriki katika
kufanikisha azma ya Tanzania kuwa nchi ya viwanda leo Jijini Dar es
Salaam. katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole
Gabriel na kushoto ni Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN)
Dkt. Jimy Yonazi
Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya
Serikali (TSN) Dkt. Jimy Yonazi akifafanua jambo wakati wa mkutano wa
Wadau Tuzungumze uliowakutanisha wamiliki wa vyombo vya Habari
nchini kujadili nafasi ya vyombo vya habari katika kujenga Tanzania
ya viwanda. Wanaomsikiliza kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye na Katikati ni Katibu Mkuu
Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari
Maelezo Dkt. Hassani Abbas akitoa ufafanuzi kwa wamiliki wa vyombo
vya habari namna uratibu wa matangazo utakavyokuwa ukiendeshwa na
Serikali wakati wa mkutano wa Wadau Tuzungumze leo Jijini Dar es
Salaam.
Mdau wa Habari Bw. Hamza Kasongo
akifafanua jambo wakati wa mkutano wa Wadau Tuzungumze
uliowakutanisha wamiliki wa Vyombo vya Habari ambapo walijadili
nafasi ya vyombo vya habari katika kujenga Tanzania ya Viwanda leo
Jijini Dar es Salaam.
Wadau wa Habari ambao ni wamiliki wa
Vyombo vya Habari nchini wakifuatilia majadiliano yaliyokuwa
yakiendelea wakati wa mkutano wa Wadau Tuzungumze huku mada kuu ikiwa
ni kujadili nafasi ya vyombo vya Habari katika kufanikisha Tanzania
ya Viwanda leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati waliokaa) akiwa katika
picha ya pamoja na wadau wa habari mara baada ya kumaliza mkutano wa
Wadau Tuzungumze ambapo uliwakutanisha wamiliki wa vyombo vya habari
huku mada kuu ikiwa ni nafasi ya vyombo vya habari katika kuijenga
Tanzania ya Viwanda leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na: Lorietha Laurence - WHUSM
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni