Dunia inakabiliwa na janga kubwa la
kibinadamu kuwahi kutokea tangu mwaka 1945, Umoja wa Mataifa umesema
na kutoa ombi kusaidia kuepusha janga hilo.
Mkuu wa Misaada ya Kibinadamu
Stephen O'Brien amesema zaidi ya watu milioni 20 wanakabiliwa na
tishio la njaa na ukame katika mataifa ya Yemen, Somalia, Sudani
Kusini na Nigeria.
Shirika la Umoja wa Mataifa la
Kuwahudumia Watoto (Unicef) limeshaonya kuwa watoto milioni 1.4
watakufa njaa mwaka huu.
Bw. O'Brien amesema kuwa dola
bilioni 4.4 za Marekani zinahitajika ifikapo Julai mwaka huu ili
kuepuka janga la baa la njaa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni