Mario Balotelli amefunga goli lake
la 10 katika msimu huu na kuiongoza Nice kupambana kiume ikitokea
nyuma baada ya kufungwa hadi kutoa sare ya 2-2 na Caen hapo jana.
Wakati Nice ikiwa nyuma kwa magoli
2-0 ikiwa zimebakia dakika 20, Balotelli alimaliza ukame wa kutofunga
katika michezo minne kwa kufunga kwa shuti la karibu.
Dakika saba baadaye mchezaji
aliyetokea benchi Anastasios Donis anayeichezea Nice kwa mkopo
akitokea Juventus, aliachia shuti lililogonga mwamba na kutinga
wavuni.
Mario Balotelli akiwa ameuchukua mpira na kukimbia nao kuuwahisha kuuweka kati baada ya kufunga goli
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni