Polisi katika pwani ya Miami
wanakabiliana hali ngumu ya kudhibiti usalama dhidi ya maelfu ya
wanafunzi wa vyuo waliojaa kwenye Ufukwe wa Kusini baada ya
kumalizika majira ya kipupwe.
Wanafunzi hao wamekuwa wakijirusha
kwa kunywa pombe, kucheza huku wakisababisha uchafu mkubwa kwa kutupa
chupa pamoja na taka nyingine nyingi katika fukwe hiyo hali
inayochangia uharibifu wa mazingira.
Katika maeneo yote ya fukwe nchini
Marekani maafisa wa majiji wanawakati mgumu katika kipindi hiki
ambacho watu hufanyasherehe kwa wiki kadhaa wakiwa kwenye fukwe
wakinywa pombe, kucheza na kufanya mambo mengine yasiyoyakistaarabu.
Polisi walio kwenye pikipiki za magurudumu manne wakijaribu kudhibiti nidhamu ufukweni
Wanafunzi wakiwa wamepozi katika moja ya magari ya polisi wakipiga picha katika ufukwe huku Miami
Hali ya uchafuzi wa mazingita inavyoonekana kufuatia kuanza kwa sherehe hizo katika fukwe kadhaa Marekani
Polisi wakiwa katika jukumu la kujaribu kuimarisha usalama na utulivu katika fukwe ya Miami
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni