Real Madrid imefunga goli la dakika
za mwisho na kufanikiwa kuifunga Valencia kwa magoli 2-1 katika hatua
muhimu ya kuwania taji la Ligi ya Hispania ya La Liga.
Katika mchezo huo Cristiano Ronaldo
aliifungia Real, goli la kwanza na kumfanya kuwa mfungaji anayeongoza
kufunga magoli mengi katika ligi tano za juu Ulaya.
Katika mchezo huo ambao Ronaldo
alikosa penati, Valencia walisawazisha goli kupitia kwa Dani Parejo dakika ya 82, kisha
baadaye Marcelo akafunga goli la ushindi kwa Real.
Cristiano Ronaldo akiruka juu na kuupiga mpira kwa kichwa na kufunga goli la kwanza
Dani Parejo akipiga mpira wa adhabu uliopaa juu ya ukuta wa Real na kufunga goli
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni