Timu ya Barcelona imeendelea kukaa
kileleni mwa ligi ya La Liga wakati Luis Suarez akifunga mara mbili
na kuihakikishia ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Espanyol.
Uzembe wa Jose Manuel Jurado kupiga
pasi ya nyuma iliyomkuta Suarez, aliyeachia shuti lililompita kipa
Diego Lopez, uliifanya Barcelona kupata goli la kwanza.
Ivan Rakitic aliongeza goli la pili
kwa Barcelona kabla ya Suarez tena kutumia vyema makosa ya Espanyol
kufunga goli la tatu.
Luis Suarez akiuwahi mpira wa pasi mbovu ya nyuma ya Jose Manuel Jurado na kufunga goli
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni