Marekani imefanya mashambulizi ya
anga katika kambi ya jeshi la Syria katika kujibu mapigo ya tukio
linalodaiwa kuwa shambulizi la silaha za kemikali dhidi ya raia
katika mji unaoshikiliwa na waasi.
Makombora 59 aina ya Tomahawk
yamerushwa kutoka kwenye meli mbili za kijeshi kutoka bahari ya
Mediterranean.
Rais Donald Trump amesema
wameshambulia kambi ya jeshi ya Shayrat ambayo ilifanya mashambulizi
ya kemikali siku ya jumanne.
Hili ni shambulizi la kwanza la
Marekani moja kwa moja dhidi ya serikali ya Syria. Urusi ambayo
inamuunga mkono rais Bashar al-Assad, imeshutumu shambulizi hilo.
Kambi ya jeshi ya Shayrat inavyoonekana baada ya mashambulizi
Meli ya jeshi la Marekani ikirusha makombora ya Tomahawk
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni