Marouane Fellaini ametolewa nje ya
uwanja kwa kumpiga kichwa Sergio Aguero wakati timu za Manchester
City na Manchester United ambao ni mahasimu wakuu wa Jiji la
Manchester wakipambana na kutoka sare tasa katika dimba la Etihad
Stadium.
Matokeo hayo yamemuacha kocha
Manchester United, Jose Mourinho, akiwa na furaha kwa kufikisha
michezo 24 bila ya kufungwa, mafanikio ambayo yamefikiwa licha ya
Fellaini kutolewa nje ya uwanja kwa kufanya kitendo hicho cha
kizembe.
Mchezaji raia wa Argentina Aguero
nusura afunge lakini shuti lake liligonga mwamba huku kocha wao Pep
Guardiola akimaliza mchezo huo akiwa na hofu ya kipa wake Claudio
Bravo kupata jeraha na kuondolewa kwa kubebwa kwenye machela.
Marouane Fellaini akipewa kadi nyekundu kwa kumpiga kichwa Sergio Aguero
Sergio Aguero akishika kichwa akishindwa kuamini baada ya kukosa goli la wazi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni