Familia moja katika kijiji cha
Awendo katika kaunti ya Migori nchini Kenya imelazimika kufukia
kaburi baada ya ndugu yao aitwae Wilson Oluoch waliyedhani amekufa
kupatikana akinywa pombe baa.
Oluoch alikuwa hajaonekana kwa muda
wa wiki tatu na wakati akiwa hajulikani alipo ulipatikana mwili wa
mtu aliyefanana naye ukiwa umeharibika katika shamba la miwa na ndugu
zake kudhania kuwa ni yeye.
Lakini muda mfupi kabla ya mazishi
mtu mmoja aliiambia familia ya Oluoch kuwa kuna mtu wamemuona anafana
na ndugu yao kwenye baa mmoja ya karibu eneo la Rongo, na walipoenda
kumuona wakamkuta Oluoch ambaye ni dereva bodaboda akinywa pombe
zake.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni