Wakulima wa zao mirungi Kenya
watapewa msaada wa shilingi bilioni 2.2 za Kenya kutoka kwa serikali
ili kukabiliana na changamoto zinazokabili kilimo cha mirungi.
Rais Uhuru Kenyatta ameagiza
kutolewa shilingi bilioni 1.2, kama ilivyopendekezwa na timu
iliyoundwa kuchunguza matatizo ya kilimo cha mirungi ambacho Kenya ni
halali.
Kiasi hicho cha fedha kwa wakulima
wa mirungi ni nyongeza ya shilingi bilioni 1 za Kenya zilizotengwa
kwenye bajeti iliyosomwa wiki iliyopita na Waziri wa Fedha Henry
Rotich.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni