Mwanaume mmoja amekamatwa Jijini
Stockholm baada ya tukio la dereva mwenye lori kuwagonga watu na
kusababisha vifo.
Mwanaume huyo alikamatwa kaskazini
mwa jiji hilo, hajatajwa jina lake lakini vyombo vya habari vya
Sweden vinasema mtu huyo anatokea Uzbekistan.
Watu wanne walikufa na wengine 15
kujeruhiwa baada ya lori kugonga mbele ya duka.
Waziri Mkuu wa Sweden Stefan Lofven
ameliita tukio hilo kuwa ni la shambulizi la kigaidi, huku ulinzi wa
mipaka ya nchi hiyo ukiimarishwa.
Mmoja wa wahudumu wa afya akikatiza kwenye miili ya watu waliokufa
Lori lililogonga na kuuwa watu likiondolewa katika eneo la tukio
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni