Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika-Tanzania, Salome Kitomari akizungumza kwenye mkutano wa wanahabari kutambulisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Makamu Rais wa UTPC, Bi. Jane Mihanji na Mwenyekiti wa Klabu ya Waandushi Dar es Salaam akizungumza katika mkutano wa wanahabari kutambulisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 uliofanyika leo jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wanahabari na wageni waalikwa wakiwa katika mkutano na Kamati ya maandalizi ya WPFD-2017 kutambulisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo akizungumza katika mkutano wa wanahabari kutambulisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
RAIS
wa Tanzania Mh. Dk John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi
katika mkutano wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani(WPFD)
inayotarajia kufanyika mkoani Mwanza. Maadhimisho hayo ya siku mbili
yaani Mei 2 na 3, 2017 yanatarajia kuwakutanisha wanataaluma ya habari
na wadau anuai wa vyombo vya habari kujadili masuala mbalimbali ya
tasnia ya habari.
Wakizungumza leo jijini Dar
es Salaam katika mkutano wa pamoja na vyombo vya habari uliyoshirikisha
wadau mbalimbali walioshiriki kufanikisha maandalizi hayo, walisema
maadhimisho ya WPFD kitaifa yanafanyika mkoani Mwanza na yatafunguliwa
na mgeni rasmi, Rais Dk. John Magufuli pamoja na Waziri wa Habari,
Michezo, Utamaduni na Wasanii.
Akizungumza na
wanahabari, Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa
Afrika-Tanzania, Salome Kitomari ambao ni waratibu wa maadhimisho hayo,
alisema Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari yanayotarajia kufanyika
yanabeba maana kubwa kwa wanahabari na wadau wa vyombo vya Habari
Duniani kutokana na umuhimu wa tasnia yenyewe.
Alisema
vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa kwani
hakuna taifa linazoweza kuendelea na kuwa na ustawi bila ya uhuru wa
vyombo vya habari. Alisema vyombo vya habari ndivyo vinavyotoa mchango
wa kuibua uozo na hata kuleta uwajibikaji maeneo mbalimbali ambapo
serikali nayo uweza kuchukua hatua.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni