Naibu rais wa Afrika Kusini Cyril
Ramaphosa ameelezea kufukuzwa kazi kwa waziri wa fedha Pravin Gordhan
kama ni jambo lisilokubalika kabisa.
Kufukuzwa kwa waziri huyo usiku wa
Alhamisi kulisababisha kuporomoka kwa thamani ya fedha ya Afrika
Kusini randi kwa asilimia 5.
Bw. Gordhan alikuwa anaonekana kuwa
ni mpambanaji wa rushwa katika utawala ambao umekuwa ukikabiliwa na
wimbi la kukosolewa.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni