Shinikizo la kumtaka kocha Arsene
Wenger aondoke Arsenal katika majira ya joto limezidi kupamba kasi
kufuatia kupigwa kura nyingi za mashabiki wa timu hiyo zinazomtaka
afungashe virago.
Mashabiki wa Mfuko wa Arsenal
waliwauliza wanachama wa klabu hiyo iwapo wanaunga mkono hoja ya
kumpa mkataba mpya Wenger katika majira ya joto na matokeo asilimia
78 walipiga kura ya kukataa.
Kocha Arsene Wenger anatarajiwa
kusaini mkataba wa kuendelea kuinoa Arsenal kwa kipindi cha miaka
miwili licha ya ongezeko la shinikizo la mashabiki kumtaka aachie
timu hiyo.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni