Roger Federer ameshinda mchezo mkali
uliodumu kwa muda wa saa tatu dhidi ya Nick Kyrgios na kupata nafasi
ya kutinga fainali dhidi ya Rafael Nadal katika michuano ya tenesi ya
Wazi ya Miami.
Mchezaji huyo raia wa Uswizi
ameshinda mchezo huo kwa seti 7-6 (11-9) 6-7 (9-11) 7-6 (7-5) na
kufanya rekodi yake ya mwaka 2017 kufikia ushindi wa michezo 18 bila
ya kupoteza hata mmoja.
Federer atamvaa Nadal kwa mara ya 37
siku ya jumapili, na mara ya pili kwa mwaka huu baada ya kumfunga
Mhispania huyo mwezi Januari katika michuano ya tenesi ya Wazi ya
Australia.
Roger Federer akipeana mkono na Nick Kyrgios baada ya kumshinda
Roger Federer akishangilia kwa kuiangalia kamera baada ya kushinda



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni