Nchi ya China imekataza mambo
mbalimbali katika mkoa wa magharibi wa Xinjiang katika kile
ilichoeleza kuwa ni kukabiliana na vikundi vya Kiislam vyenye itikadi
kali.
Miongoni mwa mambo yaliyokatazwa ni
pamoja kufuga ndevu ndefu, uvaaji wa hijabu katika maeneo ya umma, na
kuzuia watu kuangalia televisheni ya taifa.
Xinjiang ni makazi ya jamii ya
Uighurs, ambayo ni waumini wa dini ya Kiislam ambao wamekuwa wakisema
kuwa wamekuwa wakikandamizwa.
Wanawake wa jamii ya Uighurs wakiwa wamevalia vazi la hijabu mitaani


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni