.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 25 Aprili 2017

SIR ELTON JOHN AUGUA GHAFLA NA KULAZWA AKITOKEA CHILE


Mwanamuziki Sir Elton John amejikuta akilazimika kulazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi baada ya kukabiliwa na maambukizi ya bakteria wakali na kuamua kufuta matamasha yake nchini Marekani.

Mwanamuziki huyo alijisikia kuwa mgonjwa mno mara baada ya kutoka katika ziara yake ya Amerika ya Kusuni alipowasili Uingereza akitokea Santiago nchini Chile na kupatiwa matibabu ya dharura.

Madaktari walifanya kazi ya ziada kutibu maambukizi hayo ambapo Sir Elton alilazimika kulazwa kwa siku 12, ambapo siku mbili kati ya hizo alikuwa katika chumba cha wagonjwa mahututi na kuruhusiwa kutoka Aprili 22.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni